Amka Na Fanya Mabadiliko Haya Muhimu Kwenye Maisha Yako




Image result for wake up and change

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa makala mbalimbali zinazoletwa kwenu na Scholastica Mkumbi, Natumaini uko salama rafiki yangu na unaendelea vizuri katika maisha yako. Leo ni siku nyingine ya kipekee sana kwetu katika maisha yetu hivyo tunaalikwa sote kumshukuru Mungu kwa zawadi hii ya uhai na tuitumie vizuri siku hii ya leo kuleta mabadiliko ambayo tunataka kuyaona katika dunia yetu. Mpendwa msomaji, napenda kukualika katika makala  ya leo ili tujifunze kwa pamoja mambo mazuri niliyokuandalia siku hii ya leo. Nakusihi sana rafiki ungana nami tuweze kusafiri pamoja mpaka mwisho wa somo letu la leo.

SIRI YA MAFANIKIO

Kama unatumia muda mwingi kuongea bila kuzalisha chochote mpaka siku inaisha amka na badilika anza kuzalisha leo. Upo katika hali ya madeni sugu na kuishi maisha ya kukopa kila siku amka na badilika rafiki kwani madeni sugu ndio njia nzuri ya kubaki katika umasikini. Kama unanunua vitu kwa kuongozwa na hisia badala ya akili amka na badilika sasa na usinunue vitu kwa kuongozwa na hisia. Kama wewe ni mtu wa kuishi juu ya kipato chako amka na badilika kuishi juu ya kipato chako ni njia nzuri ya kubaki kwenye umasikini. Unaishi maisha bila ya kujilipa kwanza wewe pale unapopata hela anza kujilipa leo asilimia kumi ya kipato chako.
Unaishi maisha ya mahusiano ya ndoa na uchumba halafu si mwaminifu amka na badilika acha hiyo tabia sasa. Kutokua na uaminifu katika mahusiano ni hatari sana katika maisha ya mahusiano. Familia yako haina upendo wala amani ni wakati sasa wa kuamka na kuibadilisha familia yako iwe sehemu sahihi. Wewe mwenyewe ndio una uamuzi wa kubadilisha chochote kile katika maisha yako kama ukiamua kuamka na kubadilika.
 MAMBO MUHIMU YA KUFANYA
Hatua ya kuchukua leo, rafiki, kuna mambo mengi unatakiwa kuamka na kwenda kubadilisha katika maisha yako hivyo inuka leo na nenda kabadilishe kile ambacho hakipo sawa. Wewe ndio unajijua vizuri ni sehemu gani katika maisha yako haiku sawa. Hivyo leo ni fursa kwako ya kwenda kufanya mabadiliko kwenye maisha yako katika idara zote za maisha yako.
Kwa kuhitimisha, somo limetualika sisi sote kuamka na kubadilika katika yale mambo ambayo hayako sawa katika maisha yetu. Kama ulikuwa ni mvivu hata wa kusoma kitu chochote katika maisha yako amka na badilika anza kujijengea tabia ya kujifunza kila siku kwenye maisha yako. Huwezi kufanikiwa bila kujifunza na ukitaka usipige hatua yoyote katika maisha yako endelea kukumbatia na kung’ang’ania ujinga.
Nakutakia kila la heri kwa hayo niliyokuletea,naamini yatafanya kitu katika maisha yako kama si kubadilika kabisa basi yatakusogeza katika mabadiliko.



No comments

Usiogope Kuchukua Hatua Kwa Sababu Ya Kufeli Njiani

Hasa unapotarajia kuingia Mwaka Mpya 2018 Ukweli ni kuwa hauna haja ya kuogopa kwamba ni wapi utakosea na kushindwa kwenye kile unac...