Tabia 10 Za Vijana Waliofanikiwa Kuwa Mabilionea Duniani


0x600
Wengi wetu, katika nyakati tofauti, tumewahi kujenga picha juu namna gani maisha yanaweza kuwa kama tukiwa na utajiri mwingi sana-malumu kabisa, pengine katika kiwango dola bilioni. Watu watafanya kazi maisha yao yote lakini hawafikii lengo hili , kuna baadhi ambao wanafanikiwa kulifikia lengo hili kabla hawajafika miaka thelathini. Kwa hiyo, hawa watu wanaofanikiwa sana wana kitu gani? Suzy Smith aliwahi kufanya utafiti wake na akagundua tabia kumi ambazo mabilionea wote vijana wanazo.
Anza kidogo: Mabilionea ambao hawarithi utajiri, kwa tafsiri hii, hawatoki katika famila zenye nguvu, lakini katika zile za kawaida. Mark Zuckerberg and Dustin Moskovitz walianzia katika mabweni zamani sana kabla Facebook haujawa mtandao wa kijamii mashuhuri kama ulivyo sasa. Drew Houston, mwanzilishi mwenza na CEO wa Dropbox, alianza kucheza na kompyuta alipokuwa na miaka mitano. Ni dhahiri kabisa kuwa sio lazima uanze na vingi ili utimize ndoto yako kitaaluma na kifedha.
Hali ya uharaka: Sababu ilisababisha mabilionea hawa wa thamani kufikia malengo yao mapema ni kuwa -walijua hawana muda wa kupoteza.Kuwa na ndoto bila uharaka wa kuchukua hatua si namna ya kupata mafanikio mapema. Hii ndiyo sababu Zuckerberg na Moskovitz, waanzilishi wa Facebook niliowataja hapo awali. Waliacha chuo ili watumie muda mwingi zaidi katika biashara yao mpya. Muda ni wa mhimu sana linapokuja suala la njia ya mafanikio kwa vijana.
Uvumilivu: Hii ni moja kati ya kiungo mhimu kwa aina yoyote ya mafanikio, kitaaluma,kifedha, au mengineyo. Wajasiriamali wengi waliofanikiwa huendelelea kuvumilia mambo mengi magumu, hata kama itabidi wapande juu ya vikwazo ambavyo viko kwenye njia zao. Ijapokuwa wengine hawakuwaamini au walikutana matukio ya kushindwa, mabilionea hawa vijana hawajawahi kukata tama. Kung’ang’ania bila kujali vikwazo ni ufunguo wa kufanikiwa kwa malengo yao. Elizabeth Holmes amefanya kazi bila kupumzika kwa miaka 11 kuja na njia ya kuondoa uhitaji wa kuchukua sampuli za damu wakati wa kupima damu.
Kujiamini: Kufanikiwa kwa lengo kubwa kama hilo kunahitaji kujiamini bila kujali wengine wanasema nini. Wakati kijana wa miaka 16, Sean Parker alipokamatwa kwa kosa la kuingilia mtandao wa kampuni ya Fortune 500, ni wachache sana walioona hawezi kufanyika chochote katika maisha zaidi ya kuwa mhalifu, na wachache zaidi walimuona kama mtu ambaye anaweza kuwa na mafanikio makubwa hata kuwa mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Napster. Watu wanaoishi maisha yao kwa kutegemea mitazamo ya wengine siku zote wanazuiwa na hao watu.
Viwango vya juu: Watu hawa hawaridhiki. Kwa nini niwe milionea wakati naweza kuwa bilionea? Somo kutoka kwenye kisa cha kweli-Robert Pera, aliyekuwa injinia katika kampuni ya Apple, aliiacha kampuni hiyo maridadi kabisa na kuanza ya kwake, alisema,’’Niligundua kuwa nilihitaji kuwa na mafanikio zaidi na kwa haraka zaidi’’. Ni dhahiri hakuwa na furaha na kazi ya kawaida ya uinjinia, hata kama kazi hiyo ingeonekana kuwa nzuri sana kwa baadhi ya watu. Kama mambo yanakwenda tu vizuri ila hayajawa ya kiwango cha juu sana, watu waliofanikiwa sana huwa hawaridhiki.
Fursa: Mabilionea ni hodari sana wa kutumia fursa kwa ajili ya maendeleo na mafanikio wakati wowote na kokote kule zinakojitokeza. Siku zote uwe unangalia na kujiweka katika nafasi ya kunufaika-iwe ni katika dili la kifedha, nafasi ya kujiunga na mtandao, au chochote kile kinachoweza kukusaidia kwa siku za baadae
Wanachukuliana na Hatari na Kushindwa:’’Uwe na shauku na mambo makubwa au acha kabisa’’-hii ni kauli mbiu ya watu wengi wenye mafanikio duniani. Kabla Nick Woodman, mwanzilishi wa GoPro hajafanikiwa, kampuni zake mbili za kwanza zilikufa. Shukrani kwake, aliamua kujihatarisha tena kwa mara ya tatu na akaishia kupata mafanikio makubwa. Kamwe usiogope kujihatarisha; usiogope kufuatilia thawabu kubwa.
Nidhamu Binafsi: Mafanikio makubwa huwa hayaji yenyewe. Watu ambao wamekuwa mabilionea wanafanya kazi kwa bidii na wana nidhamu, wanajiwekea kanuni ngumu za maadili ya kazi ili ndoto zao zitimie. Unapokuwa bilionea kabla haujawa na miaka 30 ni mhimu zaidi kuweka viwango vyako vya maadili bila kuchelewa. Nidhamu ni kitu mhimu sana ili uweze kufanikiwa.
Kufanya Mambo Unayoyapenda: Unahitaji tu kuwasikiliza mabilionea ambao hawakurithi mali namna walivyofanikiwa kuelewa shauku waliyonayo kwa yale wanayofanya. Shauku ni mafuta yanayowafanya mabilionea waendelee kuwaka(kufanya kazi kwa bidii) mpaka sa sita usiku na kuendelea kutoa muda wao kukamilisha lengo hata baada ya kuwa wameshapata utajiri mkubwa.
Kutumia Vipawa: Tofauti na wengi wanavyoamini, mabilionea vijana si wanadamu wenye nguvu kupita kawaida na wala hawana aina Fulani ya vinasaba ambavyo havipatikani kwa wengine. Wao ni wanadamu wa kawaida kama wengine wanaojua namna ya kutumia vema nguvu zao na kuficha madhaifu yao ili waweze kusonga mbele. Hii ndiyo dhana ya msingi. Tumia vipawa vyako.
Ni dhahiri kabisa, inahitaji mjumuiko wa tabia maalumu ili uweze kuwa na mafanikio makubwa katika eneo Fulani. Kutoka kwenye kuchukuliana na kushindwa mpaka kuinua sana malengo na nidhamu, kuna sifa nyingi ambazo wale wanaofanikiwa wakiwa vijana wanazo. Chukua kitu kutoka kwa watu hawa mashuhuri na utumie baadhi ya tabia hizi katika fani yako na maisha. Nani ajuaye, unaweza kuwa miongoni mwa watu 40 matajiri zaidi wenye umri chini ya miaka 40 kwa siku za baadae.
Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com Kujifunza Zaidi,na kama ujumbe huu umekuwa na manufaa zaidi,unaweza kushare na rafiki zako.Pia unayo fursa ya kujiunga na mtandao wa washindi ili kujifunza zaidi kupitia watsapp group bila gharama yoyote;Tuma neon “NDOTO YANGU”,Ikifuatiwa na jina lako kwenda namba 0655 720 197.
Ili kupata Makala za kila wiki za kujifunza jinsi ya kuifikia ndoto Yako,tafadhali nenda kwenye website yangu na chini upande wa kulia kwenye “weekly newsletter” andika email yako pale kisha itume.

No comments

Usiogope Kuchukua Hatua Kwa Sababu Ya Kufeli Njiani

Hasa unapotarajia kuingia Mwaka Mpya 2018 Ukweli ni kuwa hauna haja ya kuogopa kwamba ni wapi utakosea na kushindwa kwenye kile unac...