Usiogope Kuchukua Hatua Kwa Sababu Ya Kufeli Njiani
Hasa unapotarajia kuingia Mwaka Mpya 2018
Ukweli ni kuwa hauna haja ya kuogopa kwamba ni wapi utakosea na kushindwa kwenye kile unachotaka kufanya. Kama unataka kufanikiwa juu ya malengo na ndoto yako ni lazima ujifunze KUJARIBU mara nyingi zaidi hata kama umejawa na hofu kila pande nje na ndani yako.
Kumbuka ni heri kujaribu na kushindwa kuliko kutokujaribu au kufanya kabisa. Watu wanaofanikiwa katika ndoto zao huwa ni watu wasiokubali kukwamishwa na changamoto mbalimbali zilizowazunguka, bali huwa ni watu wa kujaribu mara nyingi hadi pale watakapoona matokeo fulani yanatokea juu yao.
Kama una jambo lolote ulilokuwa ukitaka kulifanya 2017 na hadi sasa ujachukua hatua ya kulifanya kwa hofu ya kufeli, nakusihi mwaka 2018 amua kulifanya ukiwa na hofu yako hivyo hivyo. Kumbuka utakapoanza kulifanya jambo hilo pamoja na hofu uliyonayo, basi ile hofu uliyonayo ndani yako itaanza kupungua na badae kuondoka kabisa ndani yako kutokana na kuamua kuchukua HATUA.
Mwaka 2018 amua kuanza safari ya kuishi na kufuata ndoto yako ili uweze kuzaa matokeo makubwa kwenye maisha yako.
Nawatakia Mwaka Mpya Mwema woote!!
2018 ukawe mwaka wa tofauti kwa kuanza na KUJARIBU na kuchukua HATUA
Believe It’s Possible!
Post a Comment