HARAKATI ZA VIJANA KUJIKOMBOA KUTOKA KATIKA UMASKINI
Kijana ni nina?
Katika nchi yetu ya Tanzania neno Kijana linatafsiriwa ni mtu wa miaka 15 hadi 39 . kipindi hiki cha maisha kwa undani ni kipindi kizito katika maisha ya mwanaadamu . Mabadiliko makubwa ya kimaumbile hutokea sambamba na kukomaa kwa mawazo.Ni kipindi cha mpito kutoka utoto kuelekea uzee.Ni kipindi chenye heka heka nyingi kwa vijana kutokana na mabadiliko ya kimaumbile,kwani kijana hutaka kujionyesha kwamba yeye ni nani katika jamii.
Hapa ndiyo msingi wa maisha ya uzeeni.Na pia ndiyo msingi wa maendeleo
ya taifa kwani vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Leo nataka
tuangalie Kikundi cha Vijana cha Tujikomboe kinachopatikana katika Kata ya
Gallapo,Kijiji cha Hallu,Wilaya ya Babati Vijijini katika Mkoa wa Manyara
baadhi ya Vijana wa Kikundi cha Tujikomboe kinachopatikana Kijiji cha Hallu ,Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara na bidhaa yao wanayoitengeneza ya chakula cha kuku |
hivyo vijana hawa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokwepo kwa masoko ya uhakika wa bidhaa yao wanayo izalisha.
Kwa kuwa wana nia ya kupambana na kujikwamua kutoka kwenye umasikini hawajakatishwa tamaa na changamoto hizo kwani bado wanazalisha bidhaa yao huku wakijaribu kujitangaza na kutafuta masoko ya uhakika kutoka kwa wadau mbalimbali
Tupe maoni yako ili vijana hawa waweze kufikia ndoto walizonazo.
Post a Comment